Kenya: Watoto wapewa haki kutumia majina ya baba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sasa watoto waliozaliwa nje ya ndoa wana halki ya kujumuisha majina ya baba zao kweney vyeti vya kuzaliwa.

Mahakama nchini Kenya imetoa uamuzi unaoruhusu majina ya baba wazazi wa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kujumuishwa kwenye vyeti vya kuzaliwa vya watoto hao bila wanaume hao kuombwa idhini.

Akitoa hukumu hiyo jaji Mumbi Ngugi alisema kuwawatoto wanaozaliwa nje ya ndoa wanakumbwa na ubaguzi.

Alisema kuwa kila mtoto ana haki ya jina la babake kuandikwa kwenye cheti chake cha kuzaliwa.

Image caption Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanamke ambaye hajaolewa anayetaka majina ya baba kuwa kwenye vyeti vya watoto wake.

Ruhusa ya baba haitahitajika jinsi imekuwa hadi sasa, ambapo unapata kuwa vyeti vingi vina herufi Xs kwenye nafasi inayostahili kujazwa jina la baba.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanamke ambaye hajaoelewa, ambaye alitaka jina la baba yao kujumuishwa kwenye vyeti vya watoto wake, akidai kuwa wanabaguliwa kwa misingi ya urithi.