Kiwanda cha mafuta chashambuliwa Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanamgambo wanasema wako kwenye kampeni ya kutaka wenyeji wa Niger Delta kupata mgao wa utajiri wa mafuta.

Kiwanda cha mafuta cha kampuni ya Chevron nchini Nigeria kimeshambuliwa na wanamgambo.

Kampuni hiyo ya Marekani inaripotiwa kufuta shughulia zake kufuatia uvamizi huo.

Kundi linalojiita Niger Delta Avengers, lililisema kuwa lililipua kituo cha umeme huku wenyeji wakisema kuwa walisikia mlipuko.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mafuta yanachangia asilimia sabini ya pato la taifa nchini Nigeria.

Avengers wanasema kuwa wako kwenye kampeni ya kutaka wenyeji wa Niger Delta kupata mgao wa utajiri wa mafuta.

Mauzo ya mafuta yasiyosafishwa yanachangia asilimia sabini ya pato la taifa nchini Nigeria, nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.