Ardhi kwa manufaa ya umma SA

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Jackob Zuma wa Afrika Kusini

Bunge la Afrika Kusini limeridhia marekebisho ya muswada ambao inairuhusu serikali kuwa na mamlaka kamili juu ya upokonyaji wa ardhi kwa maslahi ya umma.

Muswada huo hatimaye unatarajiwa kutiwa sahihi na baadaye kuwa sheria kamili na Rais Jackob Zuma, ambao itawezesha serikali kufanya manunuzi ya lazima ya ardhi ili kuharakisha mipango ya kuharakisha ugawanyaji wa ardhi.

Karibu miongo miwili sasa, baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo kupita, inakadiriwa kuwa asilimia kumi ya ardhi ya Afrika Kusini iliyokuwa inamilikiwa na wazungu imerejeshwa kwa wamiliki weusi, hata hivyo hiyo ni theluthi moja tu ya lengo la uongozi wa African National Congress.

Chama hicho kimesema kwamba kupitisha muswada huo kwa wajumbe wa baraza hilo ni sawa na enzi mpya ya ulinzidi na ugawaji wa ardhi.

Inakadiriwa kuwa itachukua wiki kadhaa ama miezi kadhaa mbele hatua ya uwekaji saini muswada huo na hatimaye kuwa sheria.