Misaada haiwafikii walengwa-UN

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Staffan de Mistura

Maafisa wa umoja wa mataifa wametoa angalizo juu ya jitihada wanazozifanya kuwafikishia misaada wahitaji nchini Syria kwamba hazifikii malengo . Mkuu wa kitengo cha misaada wa umoja wa mataifa,Jan Egeland amesema kwamba mipango ya umoja wa mataifa ni kuwafikia wahitaji milioni moja kwa mwezi wa tano pekee.

Lakini mpaka sasa watu laki moja na sitini pekee ndiyo waliofikiwa, naye mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria , Staffan de Mistura anasema kwamba wananchi wako katika hatari kubwa ya njaa vingenevyo vikosi vya serikali na makundi ya upinzani kuruhusu mashirika ya misaada ya upatikanaji rahisi.