Mke wa Gbagbo apoteza rufaa Ivory Coast

Simone Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Simone alihukumiwa kufungwa jela miaka 20

Mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Simone, amepoteza rufaa yake ya kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela dhidi yake.

Bi Gbagbo alikuwa amewasilisha rufaa hiyo katika Mahakama ya Juu nchini humo.

Alihukumiwa kufungwa jela mwaka jana kutokana na mchango wake wakati wa ghasia zilizotokea baada ya mumewe kukataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Bw Gbagbo mwenyewe anazuiliwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita mjini The Hague, Uholanzi ambapo anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita kuhusiana na machafuko hayo.

Watu zaidi ya 3,000 walifariki wakati wa ghasia hizo za baada ya uchaguzi.

Mshindi wa uchaguzi Alassane Ouattara, hatimaye alichukua mamlaka akisaidiwa na wanajeshi wa Ufaransa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bw Gbagbo na mkewe baada ya kukamatwa

Bw Gbagbo na mkewe walikamatwa na kuzuiliwa.