Bomu Uganda 2010: Wahusika wafungwa maisha Jela

Image caption Watu 5 waliohusika na shambulio la bomu nchin Uganda mwaka 2010 wahukumiwa maisha jela

Watu 5 waliopatikana na hatia ya mashtaka ya ugaidi kufuatia shambulio la bomu la mwaka 2010 katika mji mkuu wa Uganda Kampala ambalo liliwaua watu 74 wamepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela.

Miongoni mwao ni Issa Ahmed Luyima ,mpangaji mkuu wa mashambulio hayo yaliodaiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la al-Shabab.

Watu wengine wawili waliopatikana na hatia ya ugaidi walipatiwa hukumu ya kifungo cha miaka 50 jela.

Akitoa hukumu hiyo,jaji Alfonse Owiny-Dollo alisema hakuamini kwamba hukumu ya kifo itazuia visa kama hivyo.

Image caption Kiongozi wa shambulio hilo Issa Ahmed Luyima

Kupatikana kwao na hatia ni mara ya kwanza kwa washukiwa wa kundi la wapiganaji wa al-Shabab nje ya Somalia.

Watu wengine sita ambao pia walishtakiwa waliachiliwa kwa mashtaka ya ugaidi na mauaji ,lakini mmoja wao alipatikana na hatia ya shtaka la kiwango cha chini.