Waliofutwa wakataa kung'atuka madarakani G Bissau

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri mkuu mpya wa Guinea Bissau

Mawaziri kadhaa waliofutwa kazi nchini Guinea Bissau wiki mbili zilizopita wamekataa kung'atuka mamlakani.

Waziri mkuu mpya, Baciro Dja, aliapishwa hapo jana, japo baraza la mawaziri la sasa limekataa kumtambua.

Wanasema angefaa kuteuliwa na chama tawala cha ( PAIGC) na sio rais Jose Mario Vaz.

Uteuzi huo ulisababisha maandamano makubwa siku ya Alhamis.

Tangu mwaka 1974, hakuna kiongozi yeyote wa kuchaguliwa wa taifa hilo, ambaye ametumikia muhula wake kamili.