Mapigano yaibuka kati ya IS na waasi Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mapigano Syria

Mapigano makali yametokea Kaskazini mwa Syria wakati kundi la Islamic State linajaribu kutwaa mji unaodhibitiwa na waasi wa Marea.

Islamic State walitekeleza shambulio la asubuhi mapema, wakiwa na makombora, mizinga na magari yaliowekwa bomu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mtoto wa shule Syria

Kundi hilo limekuwa likikaribia eneo hilo siku za hivi karibuni.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa raia wamejipata katikati mwa mapigano hayo wakijaribu kutoroka.