Mkutano wa Trump wakabiliwa na ghasia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkutano wa Trump wakumbwa na ghasia

Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Marekani walitumwa kwenye mji wa San Diego, jimbo la California, kuzuia makabiliano kati ya maelfu ya wafuasi na wanaompinga mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump.

Waandamanji hao walipeperusha bendera za Marekani na Mexico, wakati bwana Trump akitoa hotuba yake.

San Diego, ni kilomita chache tu kutoka mpaka wa Mexico na Marekani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkutano wa Trump mjini San Diego

Bw Trump amesisitiza kuwa iwapo atachaguliwa kuliongoza taifa hilo,atajenga ukuta mkubwa ili kuwazuia wahamiaji haramu kuingia nchini humo