Zika: WHO laondoa wasiwasi katika Olimpiki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mji wa Rio de Jeneiro

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa limeingilia kati katika kukabiliana na virusi vya Zika huku kukiwa na wito kwa mashindano ya michezo ya Olimpiki kuahirishwa kufuatia mlipuko wa virusi hivyo.

Afisa wa WHO Bruce Aylward ameiambia BBC kwamba hatua za kukabiliana na ugonjwa huo zimekamilishwa.

Haki miliki ya picha .
Image caption Watoto walioathirika na Zika

Alikiri kwamba shirika la afya duniani WHO linaweza kufanya kazi nzuri zaidi kupitia kutoa tangazo kuhusu kile kinachoendelea na kwamba hakuna haja ya kuahirisha michezo hiyo.

Katika barua ya wazi wanasayansi 152 walisema kuwa utafiti waliofanya kuhusu Zika umeonyesha kuwa ni hatari kwa michezo hiyo kuendelea.

Image caption Wanasayansi wataka mashindano ya Olimpiki kuahirishwa

Pia wamesema kuwa shirika hilo la afya duniani linafaa kufuata maelezo yake kuhusu Zika.

Ugonjwa huo unahusishwa na watoto walio na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa afya wakabiliana na Zika

Kati ya Februari na Aprili,Brazil ilisajili zaidi ya visa 90,000 vya Zika.

Visa vya watoto waliohusishwa na virusi hivyo ni 4,908 kufikia mwezi Aprili.