Zika: Wataalam wataka michezo kuondolewa Brazil

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rio Olimpiki

Zaidi ya wanasayansi 100 maarufu duniani wametaka michezo ya Olimpiki kuondolewa nchini Brazil ama ihairishwe kutokana na hatari ya virusi vya zika.

Michezo hiyo imeratibiwa kung'oa nanga tarehe tano mwezi agosti.

Ni takriban miezi mitatu ilosalia kabla ya michezo ya olimpiki kuanza mjini Rio de Janeiro nchini Brazil.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uwanja wa michezo ya Olimpiki mjini Rio

Wataalam 150 wanasema zaidi ya wanariadha na mashabiki laki tano huenda wakakabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi vya Zika.

Brazil imekuwa kitovu cha janga hilo la Zika, na japo hausababishi kifo katika baadhi ya kesi, huwa unasababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo wao kudumaa.

Wanasayansi wanasema huenda virusi hivyo vikasambazwa katika maeneo maskini duniani kama vile Afrika na bara Asia, wanariadha na mashabiki wakirejea kutoka Rio.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwenge wa michezo ya Rio

Katika barua yao, wamesema kuwa matukio mengine yameahirishwa kutokana na sababu sawa na walioelezea, na kuwa WHO ina mgongano wa maslahi, kutokana na ushirikiano iliyo nao na kamati ya kimataifa ya Olimpiki.

Brazil inasema imeweka mikakati ya kuangamiza mbu anayesambaza maradhi hayo.