Fiji kuondoa wanajeshi wake Sinai, Misri

Image caption Wapiganaji wa kiislamu wamekuwa wakifanya mashambuzili Sinai

Kamanda mwandamizi wa jeshi la Fiji, amesema askari wa kuweka amani wa Fiji kaskazini mwa Misri, katika rasi ya Sinai, wanapunguzwa kwa sababu hali ya usalama huko imeharibika.

Kamanda Humphrey Tawake, amesema nusu ya wanajeshi wa Fiji, waliomo kwenye kikosi cha kimataifa, wameshaondoshwa katika maeneo ya hatari ya Sinai, na vituo kadha vya mbali vimefungwa, katika majuma machache yaliyopita.

Wakuu wa ulinzi wa Marekani, walitangaza mwezi uliopita, mpango wa kupunguza wanajeshi wa Marekani huko Sinai.

Wapiganaji wa Kiislamu wamekuwa wakifanya mashambulio huko, kwa muda mrefu.