Iran haitapeleka raia wake kuhiji Mecca

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mecca

Waziri wa utamaduni nchini Iran anasema kuwa nchi hiyo haitawatuma raia wake kwenda kuhiji mwaka huu nchini Saudi Arabia.

Ali Jannati alisema kuwa sio vizuri kwa Saudi Arabia kuwawekea vizuizi raia wa Iran wanaotaka kuhiji.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mamia ya watu waliuawa kwenye mkanyagano mwaka uliopita

Wakati wa hija ya mwaka uliopita, mamia ya mahujaji waliuawa wengi wao raia wa Iran wakati wa kisa kibaya cha mkanyagano.

Msukosuko kati ya Iran na Saudi Arabia umekuwa ukiongezeka wakati pande hizo mbili zinaunga mkono makundi tofauti yanayopigana nchini Syria na Yemen.