Wazazi wamtelekeza mtoto makusudi Japan

Haki miliki ya picha Juliancolton
Image caption Wazazi wanasema walimtelekeza mwanao kama njia ya kumuadhibu.

Wazazi wa mtoto mvulana wa umri wa miaka saba ambaye hajulikani aliko katika milima iliyo kaskazini mwa Japan wamekiri kuwa walimtelekeza mvulana huyo kama njia ya kumuadhibu.

Mtoto huyo hajaonekana kwa muda wa siku mbili tangu wazazi wake, wamuache katika eneo la Hokkaido, ambapo wanaishi wanyama pori wakiwemo dubu.

Awali wazazi wake waliwaambia polisi kuwa mvulana huyo alitoweka wakati walikuwa wakitafuta mboga msituni.

Lakini baadaye walikiri kumtelekeza mwanao na kusema kuwa waliporudi kumtafuta dakika tano baadaye walipata ametoweka.