Simeone kutafakari hatma yake Atletico Madrid

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Diego Simeone

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anasema ataanza kutafakari kuhusu kuendelea kukiongoza klabu hicho baad ya kushindwa siku ya Jumamosi.

Atletico ilishindwa na Real Madrid kwa mabao 5-3 kwa mikwaju ya penalti, baada ya mechi hiyo iliyochezawa uga wa San Siro kumalizika kwa sare ya bao moja.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Atletico walishindwa na Real Madrid kwa mabao 5-3.

Hii ni mara ya pili ndani ya misimu mitatu, mbapo Atletico Madrid imepoteza kwa mahasimu hao wao wa kombe La Liga kwenye fainali.

"Kupoteza mara mbili ni kushindwa, alisema raia huyo wa Argentina ambaye ameingoza Atletico tangu mwaka 2011.

Kando na kufanikiwa kufika fainali ya ligi kuu barani ulaya mara mbili, Atletico imeshinda kombe la Copa del Rey, Europa League, Uefa Super Cup na Spanish Super chini ya uongozi wa Diego Simeone.