Takriban 17 wafariki kwenye ajali ya moto Ukrain

Image caption Watu 17 wateketea kwenye moto mjini Kiev, Ukrain.

Takriban watu 17 wanahofiwa kufariki baada ya moto mkubwa kutokea katika jumba moja la makaazi ya kuwahudumia wakongwe, karibu na mji mkuu wa Ukraine, Kiev.

Wakuu wanasema kuwa idara ya huduma za kuwaokoa watu ilifaulu kuwaokoa watu wengine 17, watano kati yao wamekimbizwa Hospitalini, wakiwa na majeraha mabaya ya moto.

Taarifa kutoka huduma ya zima moto mjini humo, zinasema kuwa moto huo ulitokea mapema leo Jumapili, katika jumba moja la kibinafsi lililoko karibu na makao hayo, ambayo yalikuwa yakiwahudumia kwa muda watu 35, kutoka katika kijiji kimoja kilichoko hapo karibu.