Uamuzi wa kesi ya Hissenne Habre kutolewa

Haki miliki ya picha
Image caption Hissene Habre

Mahakama mmoja nchini Senegal inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Chad Hissenne Habre.

Ni kesi ya kwanza ulimwenguni , kwa mahakama ya nchi kumshtaki kiongozi huyo wa zamani kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu.

Mwendesha mashtaka katika mahakama maalum ya Afrika, ambayo iliundwa na Umoja wa Afrika mjini Dakar ametoa ombi la kumtaka Habre kufungwa kifungo cha maisha.

Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake miaka ya 80, madai ambayo ameyakana

Habre alikamatwa nchini Senegal , na kupelekwa uhamishoni mwaka 2013.