Marufuku ya kupasua vitabu yatolewa China

Haki miliki ya picha XINHUA
Image caption Wanafunzi nchini China

Wanafunzi wa sekondari huko China wamepigwa marufuku ya kupasua vitabu na kupiga kelele kabla ya kufanya mitihani ambayo hubainisha iwapo watajiunga na vyuo vikuu au la.

Chombo cha habari cha serikali ya China kimesema, marufuku hiyo ilitolewa na kitengo kinachosimamia elimu cha Xiamen, siku 10 kabla ya mitihani ya kitaifa ya kujiunga na taasisi mbalimbali.

Vyuo vya sekondari vinastahili kutafuta mbinu mbadala za miongozo ya kisaikologia , Gazeti la vijana la China limeripoti.

Mitindo hiyo ya upasuaji vitabu na upigaji kelele imeshuhudiwa kwa miaka mingi iliyopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanafunzi nchini China

Maafisa wa Xiamen, wamehimiza mashule kuwaruhusu wanafunzi kupunguza msongamano wa kiakili ' kwa njia bora za kiafya' bila vigezo vyovyote.

Zaidi ya wanafunzi milioni kumi kote nchini China hufanya mtihani huo wa siku mbili unaodaiwa kuwa mgumu zaidi.

Mtihani huo kwa jina Gaokao hubaini iwapo mwanafunzi huyo atajiunga chuo kikuu.