Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wafukuzwa

Image caption Chuo kikuu cha Dodoma

Wanafunzi katika chuo kikuu cha Dodoma nchini Tanzania wamefukuzwa chuoni humo baada ya kuzuka kwa mgogoro kati ya serikali na wahadhiri wa chuo hicho.

Wanafunzi hao waliagizwa kuondoka katika chuo hicho kufikia saa kumi na mbili jioni siku ya Jumapili.

Image caption Ilani

Ilani hiyo imesema kuwa kulikuwa na makosa katika mafunzo ya wanafunzi wanaosomea shahada ya elimu ikiwemo sayansi,hesabati,teknolojia hivyobasi serikali imewataka wanafaunzi hao kuondoka chuoni humo hadi ilani nyengine itakapotolewa.

Maelezo kuhusu mgogoro huo kati ya wahadhiri wa chuo hicho na serikali hayajulikani.