Mashambulizi ya kujitoa mhanga yaua 20 Iraq

Haki miliki ya picha Reuters

Wanamgambo wa IslAmic state wameendesha misururu ya mashambulizi ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari ndani na nje mwa mji mkuu Baghdad ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 20.

Mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga alilenga kizuizi cha kijeshi katika eneo lenye washia wengi la Shaab.

Haki miliki ya picha AP

Shambulizi lingine lililenga soko katika mji wa Tarmiyah kaskazini mwa Baghdad.

Watu kadha wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.

Islamic State imeongeza mashambulizi ya kujitoa mhanga mjini Baghdad miezi ya hivi karibuni, wakati ikikabiliwa na mashambulizi ya serikali kwenye jitihada za kukomboa maeneo wanayoyadhibiti.