Mapigano yachacha mashariki mwa Ukrain

Haki miliki ya picha BBC World Service

Kumekuwa na mashambulizi zaidi mashariki mwa Ukrain kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaounga mkono Urusi, huku ripoti zikisema kuwa wanajeshi watatu wa Ukrain wameuawa.

Mapigano yamekuwa yakichacha wiki yote ambapo wanajeshi watano wa Ukrain waliuawa siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha

Msemaji wa jeshi la Ukrain alisema kuwa mapigano mengi yalitokea eneo la Donetsk na mji unaodhibitiwa na serikali wa Mariupol.

Muungano wa Ulaya utaamua wiki zinazokuja ikiwa utaendeleza vikwazo dhidi ya Urusi, ambayo inalaumiwa kwa kuendesha uchokozi dhidi ya Ukrain.