Marekani: Magaidi wanalenga Euro 2016

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Euro2016

Marekani imeonya kwamba michuano ya soka ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao huenda ikalengwa na wapiganaji.

Idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Ulaya katika miezi ya kiangazi watavutia mashambulio kutoka kwa wapiganaji hao,idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imesema.

Kinyang'anyiro hicho kitaandaliwa kuanzia mwezi Juni 10 hadi tarehe 12 Julai katika maeneo tofauti.

France imewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia shambulio la Islamic State mjini Paris.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Timu ya Wales

Katika tahadhari yake ya kusafiri iliotolewa kwa raia wake, wizara hiyo imeonya kuhusu hatari ya mashambulio ya wapiganaji hao barani Ulaya.

Mshambulio hayo yanaweza kulenga maeneo ya kitalii,migahawa,vituo vya kibiashara na uchukuzi.