Afisa wa serikali ajuta kubofya 'like' India

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Afisa wa serikali ajuta kubofya 'like' India

Afisa mmoja mkuu serikalini amejipata anajuta baada ya kubofya kitufe cha ''like'' kwenye taarifa inayokosa waziri mkuu wa India kwenye ukurasa mmoja wa Facebook.

Afisa huyo wa jimbo la Madhya Pradesh amejipata taabani baada ya kuandikiwa barua ya kushushwa madaraka na kuhamishwa .

Yamkini Ajay Gangwar alibofya like na kwenye taarifa iliyokosoa sera za waziri mkuu bwana Narendra Modi.

Gangwar anakashifu hatua kali zilizochukuliwa dhidi yake kwa ''kosa hilo dogo'' akiitaja kuwa vita vya kisaikolojia.

Hatua hiyo kali imewadia wakati umma na wanaharakati wa haki za kibinadamu wanasema kuwa uhuru wa kujieleza nchini humo umeanza kutishiwa na sera za serikali.