India yaanzisha huduma ya kusambaza maji matakatifu

Haki miliki ya picha NLP
Image caption Mto Ganges

Serikali ya India imesema kuwa inajiandaa kuzindua huduma za kusambaza maji matakatifu na chakula kupitia ujumbe.

Waziri anayesimamia huduma ya kutuma ujumbe ya posta Ravi Shankar Prasad amesema kuwa maji kutoka kwa maeneo takatifu katika mto Ganges yatapatikana kupita ujumbe utakaotumwa pamoja na katika mitandao mingine.

Mto Ganges unaheshimiwa na watu wa jamii ya Hindu ambao ndio wengi na maji yake hutumika katika hafla za kidini.

Pia alitangaza mpango wa kutoa chakula kitakatifu kinachojulikana kama Prasad kutoka kwa mahekalu ya kihindi.