Vikosi vya Iraq vyapata upinzani mkali wa IS

Image caption Vikosi vya Serikali ya Iraq vyapambana vikali na IS

Vikosi vya Serikali ya Iraq vimekutana na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State wakipigania mji wa Falluja, takriban kilometa 15 magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Baghdad.

Vikosi vya Iraq vinavyoungwa mkono na wanamgambo wa kishia, wamekuwa wakifanya jitihada kwa kipindi cha siku nane ziliopita, lakini bado hawajafanikiwa kuuzingira mji wote.

Wanajeshi wa Iraq wanasema walirudisha mahambulizi dhidi ya IS, mashambulizi yaliyoanza alfajiri.