Njama ya pasipoti Malaysia yatibuka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Njama ya pasipoti Malaysia yatibuka

Serikali ya Malaysia imewaachisha kazi maafisa 15 wa forodhani, wanaotuhumiwa kuwa sehemu ya genge la watu lililohujumu mtandao wa serikali unaotumiwa kutathmini historia ya wasafiri wanaoingia na kutoka nchini humo.

Maafisa hao wanatuhumiwa kutatiza mfumo wa kompyuta ya serikali inayochunguza na kuhifadhi rekodi ya idara ya uhamiaji kwa miaka miwili na kuwaruhusu baadhi ya wasafiri kuingia nchini humo bila kutambuliwa.

Njama hiyo iligunduliwa baada ya mtandao huo mzima wa kompyuta katika viwanja vya ndege kutatizika mara kadhaa katika siku mmoja.

Wakuu wanasema kwamba swala la mara kwa mara la kutatizika kwa mitandao hiyo inaashiria bayana kuwa ni njama mahsusi iliyosadifiana na kuwasili kwa baadhi ya ndege uwanjani humo.

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Mji mkuu wa Malaysia

Maafisa wengine 65 wamehamishwa huku kikosi maalum kikiundwa kupiga msasa shughuli katika viwanja hivyo.

Uchunguzi umebaini kuwa takriban maafisa 100 wa forodhani walihusika katika njama hiyo.

Ulanguzi wa magenge ya biashara ya watu au makundi ya kigaidi huenda yanalipa pesa ili kupitishwa katika milango ya uwanja wa ndege bila ya kujulikana au kuficha historia yao ya ujangili.