Besigye: Upinzani wafanya mgomo mahakamani

Image caption Kizza Besigye

Upinzani umefanya mgomo katika mahakama moja ya mjini kampala kupinga hatua ya upande wa mashtaka ya kushindwa kumuwasilisha kiongozi wao Kizza Besigye ambaye ameshtakiwa na uhaini.

Upande wa mashtaka unasema bw Besigye hakuweza kuwasilishwa mahakamani kutokana na tishio la kiusalama.

Hakimu wa mahakama hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 15 mwezi Juni ili kuangazia ombi la upande wa mashtaka kusikiliza kesi hiyo katika mahakama iliopo karibu na jela ambayo Besigye anazuiliwa.

Bw Besigye alishtakiwa kwa mashtaka ya uhaini baada ya chama chake cha FDC kusema kuwa kimemuapisha kama kiongozi wa Uganda,kikikana ushindi wa rais Museveni mnamo mwezi Februari kama uliojaa udanganyifu.