EgyptAir: Sauti zilisikika katika kisanduku cheusi

Haki miliki ya picha Egyptian armed forces
Image caption vifusi vye ndege ya EgyptAir

Ishara zinazodaiwa kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya EgyptAir ilioanguka mwezi uliopita zimepatikana kulingana na wapelelezi wa Misri.

Taarifa zinasema kuwa zilipatikana na meli moja ya Ufaransa iliokuwa ikifanya usakaji katika bahari ya Mediterenean.

Kulikuwa na watu 66 walioabiri ndege hiyo aina ya Airbus 320 ilioanguka mnamo mwezi Mei tarehe 19 wakati ilipokuwa ikipaa kutoka Paris kuelekjea Cairo.

Ilipotea katika rada ya Ugiriki na Misri bila ya kutuma ujumbe wowote wa tahadhari.Hakuna maneno yoyote kutoka kwa mamlaka ya Ufaransa kuhusu yaliotokea.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege ya EgyptAir

Maafisa wa Misri wanasema kwamba wiki iliopita ishara kutoka kitengo cha dharura zilipatikana lakini baadaye wakasema zilipatikana katika siku ya kuanguka kwa ndege na hazikuwa mpya.