Reli ndefu zaidi ya chini yazinduliwa Uswisi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Reli ndefu zaidi ya chini yazinduliwa Uswisi

Njia ya reli ya chini kwa chini ambayo ndio ndefu zaidi duniani na iliyoko kwenye kimo cha chini zaidi chini ya ardhi imefunguliwa leo nchini Uswizi.

Njia hiyo ya chini ya milima ina urefu wa kilomita 57 kuanzia Gotthard iliyoko Kaskazini ikipitia chini ya vilele vya milima ya Swiss Alps iliyoko kusini mwa bara ulaya.

Kabla ya kuzinduliwa kwake, kivukio cha chini kwa chini cha Seikan kilichoko Japan chenye urefu wa kilomita 53.9 km ndicho kilichokuwa chenye urefu mkubwa zaidi duniani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Reli hiyo inapigiwa upatu kubadilisha kabisa mfumo mzima wa usafiri wa mizigo barani Uropa.

Aidha kivukio kati ya Ufaransa na Uingereza cha Channel Tunnel chenye urefu wa kilomita 50.5 km ndicho kinachoorodheshwa cha tatu kwa urefu duniani.

Reli hiyo inapigiwa upatu kubadilisha kabisa mfumo mzima wa usafiri wa mizigo barani Uropa.

Mizigo na kontena zinazobebwa na mamilioni ya lori ya mizigo sasa itakuwa inabebwa kwa treni zinazoenda kasi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashine iliyotumika kuchimba njia hiyo ya chini kwa chini ina urefu sawa na viwanja vinne vya soka.

Ujenzi wake umechukua takriban miaka 20, na imegharimu zaidi ya dola bilioni 12 za Marekani.

Mashine iliyotumika kuchimba njia hiyo ya chini kwa chini ina urefu sawa na viwanja vinne vya soka.

Viongozi wakuu barani ulaya wanatarajiwa kuhudhuria kuzinduliwa kwa njia hiyo mpya ya usafirishaji mizigo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahandisi walichimba kilomita 2.3km chini ya ardhi kabla ya kuanza kazi yao iliyozoa tani 28 za mawe na mchanga.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, Francois Hollande wa Ufaransa na waziri mkuu wa Utaliano Matteo Renzi watajiunga na viongozi wa Uswisi katilka hafla hiyo.

Wahandisi walichimba kilomita 2.3km chini ya ardhi kabla ya kuanza kazi yao iliyozoa tani 28 za mawe na mchanga.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Njia hiyo ya chini ya milima ina urefu wa kilomita 57 kuanzia Gotthard iliyoko Kaskazini ikipitia chini ya vilele vya milima ya Swiss Alps iliyoko kusini mwa bara ulaya.

Wahandisi 9 walipoteza maisha yao wakifanya kazi chini ya milima hiyo ya Alps.

Itakapoanza shughuli yake rasmi mwezi Desemba, reli hiyo ya chini kwa chini itawawezesha watu na mizigo kusafiri kati ya Zurich nchini Uswisi na Milan Italia wakitumia muda wa saa 2 na dakika 40 pekee.