Kenya kuwaondoa wakimbizi

Haki miliki ya picha
Image caption Kambi ya wakimbizi nchini Kenya

Serikali ya Kenya imepanga kufunga kambi zote za wakimbizi mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri wa maswala ya usalama wa taifa bwa Joseph Nkaisserry amesema zaidi ya watu laki sita ambao kwa sasa wanaishi katika makambi tofauti,watarejeshwa makwao.

Miongoni mwao wameishi katika kambi hizo kwa zaidi ya miaka 25.

Serikali ya Kenya inasema wakimbizi wanasababisha mzigo wa kiuchumi huku wakihatarisha usalama.

Watetezi wa waki za binaadamu wamekosoa wazo hilo na kusema Kenya watatengeneza mazingira magumu.