Wanajeshi wanaowacha kuvuta sigara kuzawadiwa

Haki miliki ya picha
Image caption Wanajeshi wa Korea Kusini

Korea Kusini imezindua kampeni mpya inayowapatia wanajeshi zawadi nyingi iwapo watawacha kuvuta sigara.

Wizara ya ulinzi inatumai kwamba itashinikiza kikosi chote kuwacha tabia hiyo kwa pamoja wakiahidiwa likizo ya zaidi iwapo kila mwanajeshi atawacha kuvuta sigara kulingana na kituo cha habari cha Yonhap.

Pia kutakuwa na zawadi taslimu ya dola 3,360 kwa vitengo vitakavyofanikiwa katika juhudi zao za kukabiliana na uvutaji sigara.

Wizara hiyo imesema kuwa itatoa vifaa vya kujivinjari kama vile meza za mchezo wa pool.

Haki miliki ya picha smoking.soldiers
Image caption Wanajeshi wanaovuta sigara kuzawadiwa Korea Kusini

Wizara hiyo imetaja utafiti uliofanywa 2015 ambao ulisema ni asilimia 40 wa wanajeshi wanaovuta sigara ikilinganishwa na asilimia 35 ya wanaume wa Korea walio katika umri wa miaka 20.

Utafiti huo ulisema kuwa watu wengi huanza kuvuta sigara kila siku wanapojiunga na jeshi.Maafisa wanasema kuwa uvutaji sigara unafaa kupunguzwa hadi asilimia 30.