Wanane wauawa kikatili Tanga, Tanzania

Image caption Tanga, Tanzania

Uchunguzi kuhusiana na mauaji ya kutisha yaliyojaa utata unaendelea kufuatia kuuawa kwa watu wanane mkoani Tanga Tanzania.

Mauaji hayo yamekuja wiki chache kufuatia mengine yaliyotokea katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Pwani.

Kuhusiana na mauaji ya Tanga, Kamanda wa polisi mkoani humo Leonard Paulo amesema watu wanaohofiwa kuwa ni majambazi waliwateka wakaazi wa Kitongoji cha Mabatini wilayani Tanga kutoka majumbani kwao na kuwaua kwa kuwakata kata na mapanga.

Mauaji hayo yalifanyika karibu na eneo ambalo liko jirani na Mapango ya Amboni, ambapo Februari mwaka jana kulitokea mapigano yaliyosababisha vifo ikiwemo askari polisi mmoja.

Habari zinasema wauaji katika tukio hilo la Tanga walijitambulisga kama.

Akisimulia maauaji hayo yalivyotokea mke wa mmoja ya waliouawa alisema wakatio wakiwa wamelala waligongewa na watu wasiojulikana ambao walijitambulisha kama askari na kumnchukua mume wake na kumtaka wampeleke kwa kaka yake ambaye pia walimuuuapamoha na watu wengine.