Mhariri wa Korea Kaskazini amsifu Trump

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimemsifu mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump kuwa mwanasiasa ''mwenye hekima'' ambaye anaweza kuwa na ushirikiano mzuri na Korea Kaskazini.

Uhariri wa mtandao wa DPRK ulisema kwamba ni mgombea ''anayeona mbali''.

Bw Trump hivi majuzi alisema kuwa alikuwa tayari kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un na pia amependekeza kuviondoa vikosi vya Marekani kutoka Korea Kusini.

Wachanganuzi wanasema uhariri huo sio sera rasmi ya taifa hilo lakini huenda unaangazia fikra za Pyongyang.

BBC Monitoring imesema kuwa DPRK ni miongoni mwa mitandao ya propaganda inayotumiwa na Korea Kaskazini.

Mtandao huo unadaiwa kuwakilisha maoni ya Pyongyang lakini mwandishi wake hajulikani.