Misaada zaidi yahitajika Syria

Image caption Ndege za kugawa misaada Syria

Marekani ,Ufaransa na Uingereza wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuanza kutoa misaada ya kibinadamu kwa maeneo yaliyoathirika nchini Syria.

Wamesema serikali ya Rais Assad imeshindwa kuheshimu muda wa mwisho, ambao ni mwezi Juni mwaka huu, kwa ajili ya usambazaji wa vifaa vya lazima kwa wahitaji.

Siku ya Jumatano msafara wa kutoa misaada ulifikia katika mji wa Daraya,ambao umezingira na vikosi vya serikali kwa takribani miaka minne hadi sasa,lakini haukuwa na vyakula.

Urusi imesema kuwasili kwa msafara huo ni hatua muhimu sana. Waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza amesema kukwama kwa misaada hiyo kunasababishwa na Assad mwenyewe.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa litakutana Ijumaa ijayo ili kujadili utoaji misaada nchini humo.