Di Matteo kuifunza Aston Villa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Di Matteo

Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Chelsea Roberto di Mateo ameajiriwa mkufunzi mpya wa klabu ya Aston Villa.

Raia huyo wa Italy anachukua mahala pake Remi Garde ambaye alifutwa kazi mnamo mwezi Machi kabla ya klabu hio kushushwa daraja kutoka ligi kuu ya Uingereza.

Di Matteo ambaye alishinda kombe la vilabu bingwa Ulaya na Chelsea mwaka 2012 atasaidiwa na aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Steve Clarke.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tony Xia

Villa pia walihusishwa na aliyekuwa kocha wa Manchester United David Moyes na meneja mpya wa Derby County Nigel Pearson ,lakini Di Matteo alikuwa chaguo la kwanza.

Klabu hiyo kwa sasa inamilikiwa na mfanyibiashara wa China Tony Xia.