Buhari kuzuru Niger Delta kuzima uhasama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Buhari kuzuru Niger Delta

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, hii leo atatembelea eneo la Niger Delta kwa mara ya kwanza tangu atwae madaraka.

Ataanzisha mpango wa kusafisha maeneo yaliyochafuliwa na kumwangika kwa mafuta.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Buhari ataanzisha mpango wa kusafisha maeneo yaliyochafuliwa na kumwangika kwa mafuta.

Hata hivyo ziara hiyo imefanyika wakati kuna uhasama mkali katika eneo hilo ambalo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mafuta nchini humo na rais Buhari ameapa kushughulikia matatizo ya wakaazi wa eneo hilo.

Wakaazi wa eneo hilo wanalalamika kuwa hawapati haki sawa ya rasilimali inayochimbwa kutoka kwenye ardhi yao.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamejiunga na kujihami na kundi moja jipya la wapiganaji, The Niger Delter Avengers.

Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamejiunga na kujihami na kundi moja jipya la wapiganaji, The Niger Delter Avengers.

Kundi hilo linadaiwa kuwa mstari wa mbele katika kushambulia mabomba ya mafuta na gesi nchini.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kundi hilo linadaiwa kuwa mstari wa mbele katika kushambulia mabomba ya mafuta na gesi nchini.

Inaaminika kuwa watu milion mbili walifariki chini ya muda wa miaka mitatu - wengi wao kutokana na ukosefu wa chakula - wakati eneo hilo lilipo jaribu kujitenga kutoka kwa Nigeria.