Misri yapokea meli ya kivita kutoka Ufaransa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meli ya kijeshi ya Misri

Misri imepokea mojawapo kati ya meli mbili za kijeshi za kisasa kutoka kwa Ufaransa katika mpango uliogharimu dola bilioni 1.

Meli hiyo iliotajwa jina la Gamal Abdel Nasser ilikabidhiwa katika sherehe magharibi mwa Ufaransa.

Meli ya pili iliotajwa Anwar Sadat,itawasili nchini Misri mnamo mwezi Septemba.

Meli zote mbili zinazoweza kubeba ndege zilitengezwa nchini Urusi lakini kandarasi hiyo ikasitishwa mnamo mwaka 2014 kutokana na mgogoro uliokuwepo mashariki mwa Ukraine.

Waziri wa ulinzi nchini Misri Sedki Sobhi ambaye alikuwa anahudhuria sherehe mjini Saint-Nazaire alikaribisha meli hiyo.