Waathirika wa moto Canada warejea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msitu ulioungua katika mji wa Fort McMurray

Wakazi waliokimbia mji wa Fort McMurray nchini Canada uliokumbwa na moto mkubwa mwezi uliopita,wameanza kurejea majumbani mwao.

Takriban watu elfu kumi na tano wanatarajiwa kurejea.

Wanaotarajia kurejea mapema zaidi ni wale ambao makazi yao hayakuharibiwa sana isipokuwa walikosa mawasiliano ya miundombinu kufika mjini,kutokana na kuungua kwa msitu uliokuwa unawazunguka.

Walilakiwa na mabango na yaliyokuwa na ujumbe wa kuwakaribisha nyumbani,sambamba na bendera kubwa za Canada zilizowekwa kwenye magari makubwa na pembezoni mwa njia.

Baadhi yao watatakiwa kusubiri kwa miezi kadhaa kutokana na makazi yao kuwa katika hali ya hatari.