Rais wa Senegal ataka imam aongezewe hukumu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Macky Sall

Rais wa Senegal Macky Sall amesema kuwa hukumu ya mwaka mmoja aliyopewa Imam na mwalimu mmoja wa shule kwa kupigania ugaidi ni hafifu sana.

Katika ziara yake nchini Ufaransa Bw Sall ameiambia radio France kwamba serikali yake itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Hapo Jana,Mahakama iliopo kusini mwa mji wa Kolda ,ilikataa ombi la upande wa mashtaka wa kumpatia kifungo cha miaka 5 Ibrahima Seye mwenye umri wa miaka 38.

Alihutubu dhidi ya Magharibi na ukubwa wa Marekani katika hotuba mnamo mwezi Septemba na wakati wa kesi yake.

''Kati ya Bin Laden na George Bush ,afadhali Bin Laden''.alinukuliwa akisema.