Umoja wa Ulaya uimarishwe:Tusk

Haki miliki ya picha AP
Image caption Donald Tusk Rais wa umoja wa ulaya

Rais wa baraza la umoja wa ulaya, Donald Tusk ,amesema kuwa kupambana na wimbi la kuupinga umoja wa huo na kusema unapaswa kuachana na ndoto za kuufunga uhusiano huo.

Amesema kuwa viongozi wa umoja wa ulaya wanatakiwa kuwa makini hususan kwa vitendo kama vile kuimarisha mipaka na kukamilisha muungano wa benki.

Akihutubia kongamano la wafanyabiashara mjini Brussels,Tusk ameonya kuwepo kwa madhara makubwa kama Uingereza itaondoka katika umoja huo.

Amewataka viongozi wa ulaya kuungana na kupambana na wale wanaotaka kuvunja muungano