Mafuriko zaidi yatishia Paris Ufaransa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mafuriko zaidi yatishia Paris Ufaransa

Utawala nchini Ufaransa uko katika hali ya tahadhari kuu baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo ya milima na kutishia kusababisha mafuriko zaidi.

Mto Seine unatarajiwa kuvunja kingo zake na kusababisha mafuriko katika muda mchache ujao.

Mabarabara kadha na reli na hata daraja chache zimefungwa katika maandalizi ya kupambana na mafuriko hayo yanayotarajiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manuel Valls alaumu tabia nchi kwa mafuriko yanayoikumba Paris

Wenyeji wa maeneo mengi yaliyochini na karibu na mto huo tayari wamelazimika kuhama makwao.

Tahadhari hiyo kuu inatokana na vifo vya takriban watu 10 katika siku tatu zilizopita nchini humo na Ujerumani ambayo pia imeathirika vibaya na mafuriko hayo.

Miji kadhaa Kusini mwa Ujerumani imeharibiwa sana na mafuriko.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Miji kadhaa Kusini mwa Ujerumani imeharibiwa sana na mafuriko.

Wafanyakazi wa umma wameweka vizuizi kadhaa katika kingo za mito na wakaazi wengine katika mji mmoja wamelazimika kutumia boti kusafiri kutoka manyumbani mwao.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ametaja hali ya hewa kama mabadiliko yanayohusiana na mabadiliko makubwa kote duniani.