Suluhu ya Israel na Palestina hatarini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgogoro kati ya Israel na Palestina

Matumaini ya kupatikana kwa suluhu ya mataifa mawili katika mgogoro wa Israel-Palestina yako hatarini,waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Marc Ayrault ameonya.

''Lazima hatua za haraka zichukuliwe'',alisema katika mkutano ulioongozwa na Ufaransa unaolenga kufufua mazungumzo ya amani.

Maafisa kutoka mashariki ya kati ,Umoja wa Mataifa,Arab League na mataifa 20 yanashiriki majadiliano hayo katika mji mkuu wa Ufaransa.

Lakini Israel na Palestina hayashiriki.Bw Ayrault amesema kuwa hatua za dharura zinahitajika ili kufufua suluhu hiyo ya kuwepo kwa mataifa mawili huru.

Ameongezea kwamba mataifa yenye uwezo mkubwa duniani yamekuwa yakitafuta njia ya kuhakikisha kuwa kutakuwepo usalama wa kudumu pamoja na ufadhili wa kupiga jeki uchumi ili kushinikiza Israel na Palestina kufufua mazungumzo ya amani ifikapo mwisho wa 2016.

Palestina imeyataja mazungumzo hayo kuwa muhimu huku Israel ikiyakosoa.