Maandamano ya upinzani kuendelea Kenya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano Kenya

Upinzani nchini Kenya umesema kuwa maandamano yake ya kila wiki yaliozua utata kuhusu marekebisho ya tume ya uchaguzi yataendelea Jumatatu ijayo baada ya kukosekana kwa mapatano.

Mwezi uliopita ,maandamano ya wafuasi wa upinzani katika mji mkuu wa Nairobi pamoja na miji mingine yalisababisha ghasia baada ya polisi kujaribu kukabiliana na waandamanaji.

Maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na maji kuwatawanya waandamanaji hao.

Katika maeneo mengine upinzani ulisema kuwa maandamano yatakuwa ya amani.

Maandamano hayo yanashinikiza kuvunjiliwa mbali kwa tume ya uchaguzi na nyengine kuteuliwa.

Upinzani unasema kuwa tume hiyo ina mapendeleo.