Miili 117 yapatikana baharini Libya

Haki miliki ya picha rina Militare via AP Photo
Image caption Boti ilizama

Shirika la Red Crescent organisation linasema kuwa idadi ya miili ambayo imepatikana katika ufukwe wa bahari magharibi mwa Libya imeongezeka na kufikia 117.

Waliofariki wanaaminika kuwa wahamiaji kutoka jangwa la sahara ambao walikufa maji wakijaribu kuelekea Ulaya.

Haijulikani ni lini walifariki.Walibebwa na maji na kuachwa katika ufukwe wa mji wa Zuwara,ambapo maboti mengi yalio hafifu baharini yanadaiwa kuondoka kueleka Italy yakiwa yamejaa wahamiaji.