Miili ya wahamiaji yapatikana:Libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji haramu wakijaribu kuvuka Baharini

Taarifa kutoka Libya zinasema kuwa miili ya watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji, imepatikana ikiwa imetapakaa katika mwambao wa bahari karibu na mji wa Zuwara.

Baadhi ya taarifa zinasema zaidi ya miili 85 imeonekana ikiwa imetapakaa. Ofisa kutoka shirika la msalaba mwekundu nchini humo anasema miili hiyo inahisiwa kwamba huenda ni ya watu kutoka ukanda wa jangwa la Sahara.

Hata hivyo imekuwa ni vigumu kujua kwamba ni lini hasa watu hao walizama.

Eneo linalozunguka mji wa Zuwara ni miongoni mwa sehemu za pwani ya Libya ambazo wahamiaji huanzia safari zao kuelekea ulaya.