Bondia Muhammad Ali alazwa hospitalini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Muhammad Ali alistaafu ndondi za kulipwa mwaka wa 1981

Bingwa wa dunia wa uzani wa juu wa zamani Muhammad Ali amelazwa hospitalini kufuatia maambikizi ya mapafu.

Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa katika hali wastani alipolazwa hospitalini.

Hata hivyo familia yake ilipendekeza alazwe hospitali kama tahadhari kwa sababu mbali na maambukizi hayo Ali anaugua kiharusi.

Bondia huyo alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu ndondi za kulipwa .

Mara ya mwisho bondia huyo mkongwe alipolazwa hospitalini ilikuwa ni Januari mwaka uliopita alipokuwa amepata maambukizi ya njia ya mkojo.

Msemaji wa familia yake hata hivyo hakuwaambia wanahabari alikolazwa wala alilazwa lini.