Wanajeshi 5 wa Marekani wafa ajalini

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi 5 wa Marekani wafa ajalini

Wanajeshi watano wa Marekani wamekufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kutumbukia mtoni mjini Texas.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa wanajeshi wengine wanne hawajulikani waliko.

Wanajeshi hao walikuwa katika mazoezi ya kijeshi wakitoka katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood.

Mji wa Texas umekumbwa na hali ya radi na mafuriki katika siku za hivi karibuni,ambapo hii imekuwa ni ajali ya tatu kulikumba jeshi la Marekani siku ya alhamisi.