Mkutano wa upinzani wazuiwa:Venezuela

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Nicolas Maduro wa Venezuela

Tume ya uchaguzi nchini Venezuela imezuia mkutano muhimu wa upinzani uliotarajiwa kutangaza kama wangeweza kuruhusu kura ya maoni juu ya mustakabali wa Rais Nicolas Maduro.

Zaidi ya watu nusu milioni walipiga kura ya kukubali uchaguzi mpya.

Wakati huohuo wananchi wa Venezuela wameendelea kufanya maandamano kuipinga serikali ambayo imesababisha mdororo mkubwa wa kiuchumi.

Baada ya kukaa kwa muda mrefu katika foleni za maduka bila kupata chakula,maandamano yalielekea katika ofisi ya Rais wakitoa ujumbe wa kutaka chakula.