Muhammed Ali aaga dunia

Aliyeluwa bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika, Muhammud Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.Kulingana na msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
Huwezi kusikiliza tena

19.22pm:Aliyekuwa bondia wa kimataifa nchini Kenya Muhammad Abdallah Kent anasema kuwa ameshangazwa na kifo cha Muhammud Ali na hakuweza kujizuia machozi yake wakati dadake alipompingia simu na kumueleza kuhusu kifo chake.Kent aliiwakilisha Kenya kutoka mwaka 1973 hadi 1986,mara ya kwanza akiwa katika uzani wa kati na baadaye katika uzani mzito.Alipigana na Ali katika pigano la raundi nne mwaka 1980 mjini Nairobi wakati Ali alipozuru Afrika kuyashawishi baadhi ya mataifa kujiondoa katika michezo ya Olimpiki ya Moscow baada ya Sovieti kuvamia Afghanistan.jJohn Nene ameandaa taarifa ifuatayo.

Image caption Mike Tyson katika tweeter

17.00pm:Aliyekuwa bingwa katika uzani wa Heavyweight Mike Tyson alimuenzi marehemu kwa kutuma ujumbe huu katika mtandao wake wa Tweeter akisema ''Mungu alikuja kumchukua bingwa wake''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama

16.30pm:Rais wa Marekani Barrack Obama ameongoza viongozi wengine katika kumuenzi Muhammud Ali.Obama amesema kuwa Ali aliushangaza ulimwengu na ,Ulimwengu umekuwa bora kwa sababu yake.Katika ujumbe wake mrefu ,Obama amesema kuwa yeye na mkewe Michelle wanaomba kwamba bingwa huyo wa zamani atalala mahali pema peponi.

In a lengthy statement, Obama said both he and wife Michelle "pray that the greatest fighter of them all finally rests in peace".

Image caption Mashabiki waliojitokeza katika mtandao wa facebook kutoa maoni yao kuhusu kifo cha Muhammud Ali
16.00pm:Baadhi ya maoni ya wasomaji wa mtandao wa bbcswahili waliomuenzi nyota huyo wa masumbwi
Image caption Ujumbe wa Rev Jesse Jackson katika mtandao wake wa Tweeter

15.30pm:Jesse Jackson:Walikataa kusikiza ushuhuda wake kuhusu dini yake.Walijaribu kumnyanyasa ,walijaribu kumuathiri kimwili na kiakili

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Floyd Mayweather

15.00pm:Floyd Mayweather Jr:Leo moyo wangu unanung'unika kwa kumpoteza mwanzilishi ,bondia hodari,bingwa na shujaa kwa vyovyote vile.Hakuna siku niliingia katka ulingo wa ndondi bila kukukumbuka ,alisema katika mtandao wa instagram.Ucheshi,uzuru wako na vyenginevyo ndio vitu tutakavyovienzi.

Image caption Ujumbe wa George foreman katika mtandao wa Tweeter

14.00pm:George Foreman:Aliyekuwa mwanamasumbwi George Foreman aliyewahi kupambana na Mohammed Ali katika mechi iliofanyika Zaire kabla ya Ali kuibuka mshindi anasema kuwa Mohammed ali alikuwa na ushawishi wa kukufanya akupende.Iwapo usingempenda angekufanyia vituko zaidi ndio uweze kumchukia zaidi.

13.00pm:Muhammad Ali alijiunga na masumbwi kwa bahati.
Image caption Muhammud Ali

Ali aliyekuwa na umri wa miaka 12 alikuwa na marafikize waktafuta peremende na porp corns za bure.Na alipogundua kwamba baiskeli yake imeibwa aliagizwa kwende chini ya nyumba aliyokuwepo katika taasisi ya mafunzo ya Columbia ambapo afisa wa polisi Joe Martin alikuwa akisimamia mpango wa ndondi.Martin alimwelezea Ali kwamba angeanza kunoa ngumi zake kwa kujifunza ndondi kabla ya kumtafuta mwizi huyo.Kwa haraka alijua vile ambavyo angejichukulia na alipofika umri wa miaka 18 alikuwa ameshinda dhahabu ya Olimpiki mjini Rome.

Image caption Holifield katika ujumne wake katika mtandao wa Tweeter

12.45pm:Evander Holyfield:Aliyekuwa bingwa wa dunia katika uzani mzito duniani Evander holyfield ni miongoni mwa waliomuenzi Muhammud Ali

Huwezi kusikiliza tena
12.30pm:Wasifu wa Muhammud Ali12.00pm:Aliyekuwa bingwa wa ndondi katika uzani mkubwa duniani Muhammud Ali amefariki.

Aliyekuwa bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika, Muhammud Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.Kulingana na msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.Alikuwa na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemekatetemeaka.Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.Alipozaliwa alipewa jina la Cassius Marcellus Clay.