Polisi 5 wauawa na Taliban Afghanistan

Haki miliki ya picha EPA

Takriban polisi watano wameuawa kwenye shambulizi lililoendeshwa na Taliban mashariki mwa Afghanistan.

Polisi katika mkoa wa Logar walisema kuwa watu wenye silaha, waliafyatua risasi kwenda kwa majengo ya bunge katika mji wa Pul-e Alam.

Kati ya wale waliouawa alikuwa mkuu mpya wa mahakama.

Watu wengine 19 wanaripotiwa kujeruhiwa.

Kundi la Taliban lilisema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo kulipiza kisasi mauaji yaliyofanywa na serikali dhidi ya wafungwa wa Taliban mwezi uliopita.